LA.txt Driver File Contents (epson18182.exe)

ÿþSEIKO EPSON CORPORATION

MAKUBALIANO YA LESENI YA PROGRAMU



MUHIMU! SOMA MAKUBALIANO HAYA YA LESENI YA PROGRAMU KWA MAKINI. Bidhaa, fonti, kiolesura na/au data ya kompyuta, ikiwa ni pamoja na vifaa vyovyote ambatani vilivyofafanuliwa kwa kuandikwa ("Programu") zinapaswa kusakinishwa au kutumiwa tu na Mwenye kupewa leseni ("wewe") kwa sharti kuwa unakubaliana na sheria na masharti ya SEIKO EPSON CORPORATION ("EPSON") yaliyowekwa katika Makubaliano haya. Kwa kusakinisha au kutumia Programu, unaonyesha kwamba unakubaliana na sheria na masharti yote yaliyowekwa katika Makubaliano haya. Unapaswa kusoma Makubaliano haya kwa makini kabla ya kusakinisha au kutumia Programu. Ikiwa hukubaliani na sheria na masharti ya Makubaliano haya, huruhusiwi kusakinisha au kutumia Programu hii.



1. Leseni. EPSON na watoa huduma wake wanakupa leseni ya muda ambayo ni ya binafsi, isiyo ya kipekee, isiyokuwa na mrahaba na isiyoweza kupewa wengine ya kusakinisha na kutumia Programu kwenye kompyuta yoyote moja au kompyuta ambazo unakusudia kutumia moja kwa moja au kupitia mtandao. Unaweza kuwaruhusu watumiaji wa kompyuta waliounganishwa kwenye mtandao kutumia Programu, maadamu uwe (a) umehakikisha kwamba watumiajii hao wote wanakubaliana na wamefungwa na sheria na masharti ya Makubaliano haya, (b) uhakikishe kwamba watumiaji wote kama hao wanatumia Programu na kompyuta na kuhusiana na mtandao ambao wanahusika tu, na (c) utafidia na kuweka EPSON yote na watoa huduma wake dhidi ya uharibifu, hasara, gharama na uwajibikaji ambao EPSON au watoa huduma wake wanaweza kupata kama matokeo ya watumiaji hao kushindwa kuzingatia na kutekeleza sheria na masharti ya Makubaliano haya. Unaweza pia kutengeneza nakala za Programu kama inavyohitajika kwa ajili ya malengo ya chelezo na kumbukumbu, maadamu iwe ilani ya hakimiliki imewekwa tena kikamilifu kwenye nakala hiyo ya kumbukumbu. Neno "Programu" litajumuisha vijenzi vya programu, media, nakala zote ulizozitengeneza na uboreshaji wowote, matoleo yaliyorekebishwa, visasisho, nyongeza na nakala za Programu ulizopewa leseni na EPSON au watoa huduma wake. EPSON na watoa huduma wake wamehifadhi haki zote ambazo hazijatolewa hapa.



2.Haki na Vizuizi Vingine. Unakubali kutorekebisha, kubadilisha au kutafsiri Programu. Unakubali pia kutojaribu kubadilisha uhandisi, kusimbua, kufungua au kujaribu kugundua msimbo chanzo wa Programu. Huwezi kushiriki, kukodisha, kupangisha, kutatiza, kutoa leseni upya au kuazima Programu. Hata hivyo, unaweza kuhamisha haki zako zote za matumizi ya Programu kwa mtu mwingine au chombo halali maadamu uhamishe Makubaliano haya, Programu, pamoja na nakala zote, visasisho na matoleo ya awali, kwa mtu au chombo hicho, na kwamba usibakie na nakala zozote, ikiwa ni pamoja na nakala zilizohifadhiwa kwenye kompyuta. Hata hivyo, baadhi ya nchi au utawala, haziruhusu uzuiaji au vikwazo vya kuhamisha Programu, kwa hivyo vizuizi vilivyo hapa juu huenda visitumike kwako.



3.Umiliki. Hati, haki za umiliki, na haki za rasilimali za akili za Programu na nakala zozote hapa zitabaki na EPSON au watoa huduma kwake. Hakuna uhamisho wowote wa hati kwako au umiliki wa Programu na Leseni hii haitachukuliwa kuwa mauzo ya haki zozote katika Programu. Programu imelindwa na Sheria za Hakimiliki za Japani na mikataba ya hakimiliki ya kimataifa, na hata pia sheria na mikataba mengine ya rasilimali za akili. Isipokuwa kama ilivyotolewa katika Makubaliano haya, huwezi kunakili Programu hii. Unakubali pia kutoondoa au kubadilisha hakimiliki yoyote na taarifa zozote za umiliki kwenye nakala zozote za Programu.



4. Ulinzi na Usalama. Unakubali kujaribu vyote uwezavyo na kuchukua hatua zozote zinazostahili kulinda Programu hii na kuhakikisha kwamba hakuna mtu asiyeidhinishwa anaweza kuifikia na kwamba hakuna nakala, chapisho, ufichuzi au usambazaji usioidhinishwa wa Programu umefanywa. Unakubali kwamba Programu ina maelezo ya thamani, ya faragha na siri za biashara, kwamba matumizi na kunakili kusiodhinishwa kunadhuru EPSON na watoa huduma wake, na kwamba una jukumu la kuweka faragha maelezo kama hayo ya thamani na siri za biashara.



5. Waranti yenye Kikomo. Iwapo umepata Programu kwa njia ya media kutoka kwa EPSON au muuzaji, EPSON inahakikisha kwamba media hiyo ambayo Programu imerekodiwa haitakuwa na dosari zozote katika kazi ya ufundi na vifaa chini ya matumizi ya kawaida kwa muda wa siku 90 kuanzia tarehe ya kuwasilishwa kwako. Ikiwa media hiyo itarejeshwa kwa EPSON au muuzaji aliyeuza kati ya siku 90 za tarehe ya kuwasilishwa kwako, na ikiwa EPSON itabainisha media hiyo kuwa na dosari na iwe media hiyo haikutumiwa vibaya, au kutumiwa katika kifaa chenye dosari, EPSON itabadilisha media hiyo, baada ya wewe kurejesha programu hiyo kwa EPSON, ikiwa ni pamoja na nakala zote za vipande hivyo. WARANTI ZOTE ZILIZODOKEZEWA KWENYE MEDIA, IKIWA NI PAMOJA NA WARANTI ZILIZODOKEZEWA ZA UUZAJI NA KUFAA LENGO FULANI, ZIMEZUIWA KWA KIPINDI CHA WARANTI YA MOJA KWA MOJA ILIYOFAFANULIWA HAPA JUU.



Unakiri na kukubali kwamba matumizi ya Programu ni juu yako kabisa. PROGRAMU IMETOLEWA "KAMA ILIVYO" NA BILA WARANTI YOYOTE YA AINA YOYOTE. EPSON NA WATOA HUDUMA WAKE HAWAHAKIKISHI NA HAWAWEZI KUHAKIKISHA UTENDAKAZI AU MATOKEO UNAYOWEZA KUYAPATA KWA KUTUMIA PROGRAMU. ILIYOTAJWA HAPA INAELEZEA MAREKEBISHO MAALUM NA YA KIPEKEE KWA UKIUKAJI WARANTI WA EPSON N WATOA HUDUMA WAKE. ISIPOKUWA KWA WARANTI YENYE KIKOMO ILIYOTAJWA, EPSON NA WATOA HUDUMA WAKE HAWAHAKIKISHI, MOJA KWA MOJA AU KWA KUDOKEZA, KUHUSU KUTOKIUKA, UUZAJI AU KUFAA LENGO LOLOTE MAALUM. Baadhi ya nchi au utawala haziruhusu kutengwa kwa waranti zilizodokezewa au vizuizi vya muda gani ambao waranti iliyodokezewa inaweza kudumu, kwa hivyo vizuizi vilivyo hapa juu huenda visitumike kwako. Waranti hii inakupa haki mahsusi za kisheria. Huenda ukawa na haki ambazo zinatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine au utawala moja hadi mwingine.



HAKUNA WAKATI WOWOTE EPSON AU WATOA HUDUMA WAKE WATAWAJIBIKA KWAKO, IWE INATOKANA NA MKATABA, KOSA LA DAAWA (PAMOJA NA UZEMBE), DHIMA KALI, UKIUKAJI AU WARANTI, UWAKILISHAJI MBAYA AU KIVINGINE, KWA HASARA YOYOTE YA MOJA KWA MOJA, INAYOTOKANA NA, AU YA BAHATI MBAYA AU MAALUM, IKIWA NI PAMOJA NA HASARA YOYOTE YA FAIDA AU AKIBA ILIYOPOTEA, HATA KAMA EPSON, WATOA HUDUMA WAKE AU MWAKILISHI YEYOTE AMESHAURIWA KUHUSU UWAJIBIKAJI WA HASARA KAMA HIYO, AU KWA DAI LOLOTE KUTOKA KWA MHUSIKA MWINGINYE YEYOTE. Hata hivyo, baadhi ya nchi au utawala, haziruhusu kutengwa au vizuizi vya hasara kwa bahati mbaya, inayotokana na au maalum, kwa hivyo vizuizi vilivyo hapa juu huenda visitumike kwako.



6. Usitishaji. Bila kuathiri haki zozote zingine ambazo EPSON inazo, Makubaliano haya yatasitishwa mara moja baada ya wewe kushindwa kufuata sheria na masharti haya. Unaweza pia kusitisha Makubaliano haya wakati wowote kwa kusanidua na kuharibu Programu na nakala zake zote.



7. Vizuizi vya Usafirishaji Nje. Unakubali kutohamisha, kusafirisha nje au kusafirisha tena nje Programu na data au maelezo yoyote ambayo uliyapata kutoka kwa EPSON au kutumia Programu bila leseni halisi chini ya sheria, vizuizi na masharti ya Japani, au sheria za utawala ambao Programu ilipatikana.



8. Sheria Inayotumika na Matoleo ya Jumla. Makubaliano haya yatasimamiwa na kufafanuliwa chini ya sheria za Japani bila kuzingatia migongano yake ya kanuni za sheria. Makubaliano haya ndiyo makubaliano kamili kati ya wahusika kuhusu Programu, na yanashinda agizo lolote la ununuzi, mawasiliano, matangazo, au uwakilishi kuhusu Programu. Makubaliano haya yatakuwa ya kufunga, na kwa faida ya wahusika hapa na waridhi wao, wateule na waakilishi wa kisheria. Ikiwa toleo lolote hapa litapatikana halitumiki au haliwezi kutekelezwa, halitaathiri uhalali wa salio la Makubaliano, ambalo litabaki halali na linaloweza kutekelezwa kulingana na sheria na masharti yake. Makubaliano haya yanaweza kurekebishwa tu kwa kuandikwa na kutiwa saini na afisa aliyeidhinishwa wa EPSON.



9. Watumiaji wa Serikali ya Marekani. Ikiwa unapata Programu hii kwa niaba ya kitengo au wakala yeyote wa Serikali ya Marekani, matoleo yafuatayo yanatumika. Serikali inakubali: (i) ikiwa Programu imetolewa kwa Idara ya Ulinzi (DoD), Programu itaainishwa kama "Programu ya Kibiashara ya Kompyuta" na Serikali inanunua "haki zilizozuiwa" tu katika Programu na waraka wake kwa kuwa neno hilo limefafanuliwa katika Kifungu cha 252.227-7013(c)(1) cha DFARS; na (ii) kama Programu imetolewa kwa kitengo au wakala yeyote wa Serikali ya Marekani kando na DoD, haki za Serikali katika Programu na waraka wake zitafafanuliwa katika Kifungu cha 52.227-19(c)(2) cha FAR au, katika kesi ya NASA, katika Kifungu cha 18-52.227-86(d) cha nyongeza ya NASA kwa FAR.





10. Muunganisho wa Intaneti. Huenda Programu ikawa na uwezo wa kuunganisha kwenye Intaneti ili kupitisha data na/au maelezo kutoka na kuelekea kwenye kompyuta yako yanayohusiana na programu ya EPSON na/au programu ambayo unatumia ("Bidhaa za EPSON") ikiwa ni pamoja na, lakini haijazuiwa kwa, maelezo ya modeli ya Bidhaa za EPSON, nchi/eneo unaloishi, hali ya Bidhaa za EPSON, n.k. Huenda EPSON ikabadilisha vipengee vya data hiyo na/au maelezo bila idhini yako ya mapema. EPSON haikusanyi maelezo yoyote yanayoweza kumtambua mtu binafsi bila kibali chako. Hata hivyo, huenda EPSON ikatumia maelezo yasiyoweza kumtambua mtu binafsi kwa malengo ya takwimu ili kuboresha kiwango cha huduma tunayotoa kwa watumiaji wetu. Ukikubali kusakinisha Programu, upitishaji wowote kutoka au kuelekea kwa Intaneti utakuwa kulingana na Sera ya Faragha ya sasa-wakati huo ya EPSON iliyotolewa katika tovuti ya Intaneti ya EPSON



11.Kusasisha Toleo la Programu. Huenda programu ikawa na uwezo wa kuunganisha kwenye Intaneti kwa seva ya EPSON au mhusika mwingine aliyekabidhiwa na EPSON ili kusasisha toleo la programu (i)kiotomatiki au (ii)na kibali chako cha mapema. Programu kama hiyo iliyosasishwa itachukuliwa kuwa Programu na itasimamiwa na Makubaliano haya.







EPSON EULA SW 10/30/2009 



Download Driver Pack

How To Update Drivers Manually

After your driver has been downloaded, follow these simple steps to install it.

  • Expand the archive file (if the download file is in zip or rar format).

  • If the expanded file has an .exe extension, double click it and follow the installation instructions.

  • Otherwise, open Device Manager by right-clicking the Start menu and selecting Device Manager.

  • Find the device and model you want to update in the device list.

  • Double-click on it to open the Properties dialog box.

  • From the Properties dialog box, select the Driver tab.

  • Click the Update Driver button, then follow the instructions.

Very important: You must reboot your system to ensure that any driver updates have taken effect.

For more help, visit our Driver Support section for step-by-step videos on how to install drivers for every file type.

server: web5, load: 1.17